| Mwalimu wa Michezo Deus Malongo (Katikati) akiwafunda wachezaji wa DSJ stars katika viwanja vya Mlimani |
MWALIMU wa michezo wa chuo cha uandishi wa habari Dar es
Salaam (DSJ) Deus Malongo amewataka wanafunzi kuhakikisha wanafanya mazoezi na kujiweka sawa
katika mazoezi ili waweze kujiweka sawa katika masuala ya michezo.
Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari
amesema kuwa michezo ni jambo la kuzingatia na kitu muhimu katika michezo ni
mazoezi yanayomfanya mwanamichezo kuwa katika
hali nzuri ya kushiriki na
kushinda.
“Mpira siku zote ni mazoezi ndiyo yanayofanya timu kuweza
kushinda hivyo kuna umuhimu wa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili
kujiimarisha na kuwa tayari kwa mashindano muda na wakati wowote “.Amesema.
Naye Ally Makame Naibu waziri wizara ya Michezo DSJ amesema
kuwa wanatambua umuhimu wa mazoezi hivyo
wamejipanga kuwa na muda wa kufana mazoezi mara kwa mara ili kujiweka sawa
kabisa .
“Tunatambua umuhimu wa mazoezi na tunathamini umuhimu wake
hivyo mkakati wetu upo wazi na kila mchezaji anataarifa juu ya kufanya mazoezi
na kushiriki mazoezi kujiweka sawa kwa ajili ya mechi na mashindano ya
kirafiki”.Amesema
No comments:
Post a Comment