Muhogo Mchungu ajipanga kivingine - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 31 October 2016

Muhogo Mchungu ajipanga kivingine

                                   
Muhogo Mchungu kulia akiwa na msanii mwenzake habari maelezo Dar es Salaam
MSANII mkongwe wa filamu nchini Tanzania Muhogo Mchungu amesema kuwa yupo chimbo akijiaandaa kutoa kitabu kitakachowafundisha watanzania wengi na kuwaburudisha wale  wanaopenda kusoma vitabu,

Msanii huyo amesema kuwa ana vipaji vingi na anatumia ili kuwapa burudani wale wanaomkubali n amewataka wawe na subira kwa kuwa mambo mazuri hayataki haraka baada ya muda kutimia kila
kitu kitakuwa sawa.

“Najiandaa kuandika kitabu changu ambacho kitakuwa ni zawadi kwa watanzania ambao wanafuatilia na kupenda kazi zangu nipo kwa ajili ya wananchi na watanzania watambue umuhimu wa kusoma vitabu ili kuongeza ujuzi zaidi”.Amesema


Aidha amewasihi watanzania kuendelea kutazama na kufuatilia filamu zake ambazo zipo sokoni na zinafanya vizuri sokoni ambapo ni pamoja na ile After death 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad