Wafanyabiashara wameitaka Serikali kuwapunguzia kodi kwa
kuwa hali ya maisha imezidi kuwa ngumu na uchumi unazidi kushuka kwa kasi kila
siku kwa wafanyabiashara kutokana na kukosa wateja wa bidhaa mbalimbali.
| Wafanyabiashara wakiwajibika kuwahfunza na kuwahudumia wateja kazini Mkoani Pwani |
Akizungumza na mwandishi wetu Hamza Kizogo mfanyabiashara amesema kuwa hali ya maisha imezidi kuwa ngumu na idadi ya wateja
inapungua kila siku kutokana na ukata unaowakabili
watanzania
“Mauzo kwa biashara yangu yameshuka kabisa tofauti na awali
kwa kuwa kila siku kunapopampazuka ni afadhali ya jana na bidhaa hasa za
matunda zinawahi kuharibika na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara”.Amesema
Naye Mama Asha ambaye ni mama lishe amesema kuwa biashara ya
chakula imekuwa ikimdodea na wafanyabiashara wengi wamekwama kuendelea na
biashara kutokana na ukata unaowakabili.
“Ukata unatumaliza na kutufanya tushindwe kujikimu vema na
hali ya kodi inatuumiza kwa kuwa tunaambiwa hapa kazi tu na fedha kwenye
mzunguko ni mdogo watu wa chini ndio tunaumia “.Amesema
Naye katibu mkuu wa Mkoa wa Pwani Shangwe Tamala amesema kuwa srikali inatambua changamoto za wafanyabiashara na inajali watu wake hivy utatuzi wa matatizo utafanywa punde,
"Tunatambua uhitaji na matatizo yanayowakibili wafanyabiashara na serikali ya awamu ya tano ni sikivu ipo kwa ajili ya watu wote na inajali hivyo tunaimani kuwa changamoto zenu zitafikishwa mahali husika na zitajadiliwa na kupewa ufumbuzi ".Amesema
.

No comments:
Post a Comment