Mtihani bado upo ndani ya mtihani - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 1 November 2016

Mtihani bado upo ndani ya mtihani

                                            
Elimu bure imefungua mwamko wa wa wazazi kupeleka watoto shule kuongeza ujuzi
HAKUNA marefu yasiyo na ncha ni msemo ulioachwa na mababu zetu nina imani walikuwa wametulia chini ya mwarobaini wakinywa kahawa na kuleta hadithi za hapa na pale baada ya
kumaliza kufanya kazi zao na mihangaiko ya hapa na pale.

Imani yao ilikuwa ikiwatuma kuwa kila wakati wa kutenda jambo kuna ulazima wa kufikiria na kutazama uwepo wa kesho na na kujipanga zaidi pale unapokwama  ili uweze kufikia malengo ni muhimu kutambua aina zote na kujitoa kwa hali na mali.

Si wote wanaotambua thamani ya muda utata mkubwa unakuja pale ambapo unakuwa umebakiwa na muda wa kawaida tu kufanya mambo mengi na makubwa hapo ndipo pumzi inaposhuka na kudhani kuwa upo dunia nyingine.

Ndugu zetu wameanza kuhitimisha safari yao ya miaka mine ya masomo baada ya mapambano yote ya siku na miaka kadhaa kwenda na kurudi nyumbani na wengine walikuwa wakiishi shuleni wapo waliokuwa wakikaa kwa marafiki.

Neno mtihani lina mitihani mingi na ni msamiati ambao ukiutaja kwa mwanaharakati yeyote lazima atapigwa ganzi na kukupa maana ambayo yeye mwenyewe anaitambua na anaielewa kwa mujibu wa uelewa wake.

Abdalah Ally miongoni mwa wanafunzi anasema kuwa anapenda sana kusoma na kujifunza mara kwa mara na siku zote anahakikisha kuwa ana kitu kipya kakipata na kuongeza katika ubongo wake na kwa watu wake a karibu.

“Najifunza siku zote kitu kipya na huwa nawashirikisha na ndugu zangu na jamaa niwapo shule juu ya umuhimu wa kujifunza mambo mapya kila siku bila kujali nipo katika mazingira gani na wakati pia ni jambo la kuzingatia”.Amesema

Anafafanua na kusema kuwa  pamoja na kupenda kwake kusoma kuna jambo linalompa wakati mgumu na linamfanya awe mpweke pindi anaposikia msamiati huo ukipenya kwenye sikio lake wakti wowote ule.

“Neno mtihani linanipa wakati mgumu na ninashindwa kusema kuwa naogopa mtihani ila napenda kusoma sipendi kufanya mtihani hasa nyakati za msimu wa kuelekea na sikukuu huwa zinanipa wakati mgumu “.

Kidato cha nne wanaanza kufanya mitihani yao kwa ajili ya kuhitimu kidato cha nne na hali hiiinawafanya wawe na ukaribu kabisa na neon mtihani kwa kuwa wamekuwa watahiniwa ndani ya chumba cha mtihani.

Historia inaandikwa kwa mara ya kwanza baada ya mchakato mzima wa serikali ya awamu ya tano kusimamia wanafunzi kupata elimu kwa shule ya sekondari na msingi bila gharama yoyote ile kwa shule za serikali.

Jamii inaimani na serikali na mpango mzima wa elimu kwa wanafunzi hivyo kwa kupitia mtihani inakuwa ni kipimo cha kwanza kwa serikali kutambua kile ilichotengeneza na kuwekeza kwa wanafunzi ambalo ndio taifa la kesho.

Licha ya changamoto zinazotokea katika sekta ya elimu bado jukumu la kijifunza na kuboreha mazingira kwa wanafunzi ni letu sote hakuna anayeweza kulikwepa na kuiachia serikali peke yake suala la kuboresha miundombinu ya elimu.

Waziri wa wizara ya elimu Joyce Ndalichako amesimama kidete kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa na ujuzi wanaopata wanafunzi ni wenye kiwango cha hali ya juu utakaoweza kutoa dira nzuri na matokeo mazuri kwa wanafunzi na wazazi.

Katika hotoba zake rais wa Tanzania amesema kuwa haiwezekani nchi kama Tanzania wanafunzi kusoma katika mazingira magumu licha ya kuwa na misitu bado wanaketi chini hili si jambo la kupuuzia na akatoa agizo kwa wakuu wa mikoa kusimamia upatikanaji wa madawati.

“Kila mkuu wa mkoa ana jukumu la kuhakikisha na kusimamia upatikanaji wa madawati nawanafunzi wakapata sehemu ya kuketi na sio kuketi chini na utajiri wa misitu upo nchini hivyo ni wajibu kusimamia na kuhakikisha tatizo linapungua”.Amesema


Elimu ni jambo la msingi na ujuzi kwa mwanadamu ni zawadi ambayo hakuna awezaye kuinya’ng’anya pindi inapokuwa imemkaa mtu mwenyewe,kila la kheri kidato cha nne msichore picha za messi wala Morinyo naamini kila kitu kitakuwa sawa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad