Wasaka tonge na maumivu ya maisha - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 1 November 2016

Wasaka tonge na maumivu ya maisha



Vijana wakiwa maskani jiji Dar es Salaam
                                                           

Harakati za mtu mweusi hazina mwisho wala mwanzo kwani tangu alipoletwa duniani alikuta wazazi wake wapo katika harakati nay eye alipokuwa akajikuta yupo ndani ya harakati.Mchana hata usiku bado pilika pilika zinaendelea kwa mwanaharakati ikitokea ukapata bahati ya kunmuuliza kulikoni mbona hivyo atakujibu kwa wepesi kabisa tena huku akicheka na kufuta jasho kwa kiganja cha
mkono na kukwambia si unajua tena mambo mengi.

Hapo ndipo utakapopigwa ganzi baada ya muda mfupi kupita yuleyule aliyekwambia mambo mengi kumkuta sehemu za starehe tena katika  hali ile ile si jambo la kumshangaa bado utapenda kujua tatitizo ni nini utamfuata na kumuuliza swali lile lile kulikoni mbona hivyo hapo sasa namna ya kukujibu itakuwa tofauti lazima anyanyue chupa yenye kinywaji baada ya muda atakwambia napunguza mawazo nawe huna budi kuondoka.

Kutahamaki  unakutana naye tena barabarani akiwa peke yake na shati kaweka begani akibadilisha lugha za kigeni kama msomi wa chuo kikuu huku akitoa lugha zisizo eleweka kwa watu walio karibu naye akiwataka wasimpe msaada tena kwani yeye anauwezo wa kifedha na ni msomi pia bado una nia ya kutka kutmbua tatizo nini naye atkuongelea lugha anayoyoijua yeye mwenyewe kasha atakwambia neon fupi litakalokuacha njia panda yani we acha tu atatikisa kicha na kuendelea kuongea lugha za kigeni’

Umefika nyumbani unaendelea kutathmini majibu uliyoambiwa na mwanaharakati mara unaskia kelele mamaaa nakufaaa jamani nisaidieni unakurupuka na kutoka nje kutambua sauti inatokea wapi unagundua kuwa ni kwa mwana harakati yuleyule unayemfkiria unaongeza spidi ili ufike eneo la tukio ili usingoje kusimuliwa unany’ong’onyea kabisa kwani mwanaharakati anamshushia kipigo mke wake kisa amechelewa kufungua mlago unapouliza kulikoni utaskia haya maisha tu.

Sasa hapo ndipo utakapokuwa umepata majibu ya maswali yako tangu pale awali mpaka mwisho kumbe harakati zote zile za mwanaharakati kujituma katika kazi usiku na mchana kwenda sehemu za starehe kufanya mambo yake bila mke wake  kuongea lugha za kigeni mithili ya kasuku na kuto hitaji msaada kwa rafikize na mwisho kumpiga kipenzi cha moyo wake kwa kosa la kwake mwenyewe ndio maana halisi ya neno maisha.

Kwa maana hiyo maisha yanaanza tangu ile siku unayoletwa duniani na kadri unavyozidi kukua ndivyo unavyozidi kuwa mwanaharakati kwa kufuata nyayo za wale waliokutangulia kama ndo hivyo mpaka hapo kuna haja ya wale waliokutangulia na wle unaowafuata nyayo zao kukupa wewe mbinu mbadala ili uepuke yale ambayo wao wameyafanya na baadae kuwaingiza katika matatizo kama mwanaharakati.

Maisha yanahitaji umakini mkubwa katika kila hatua unayopitia haijalishi upo wakati gani uwe wakati wa kucheka ama wakati wa kulia bado unatakiwa kuwa makini ili uweze kuvuka katika hatua hiyo salama salmini achana na ile kasumba ya kufikiria kulala maskini na kuamka tajiiri hizo ni ndoto za Abunuwas ambaye hata yeye zilimshinda kuziota akaamua kuamka kuendelea na shughuli nyingine.

Kukurupuka na kufanya maamuzi katika maisha kutakufanya upoteze dira na kuanza kuyumba mithili ya Ngoswe hali itakayokufanya upoteze na kushusha hadhi yako katika jamii jichunge katika kila hali na kila jambo unalolifanya itengeneze leo vizuri ili iwe rahisi kwa wale watakaokufuat kesho’
Maisha ni kitu ambacho kipo kwa kuwa ulikikuta pia utakiacha kwa kuwa hakina tatizo na wewe hakuna mwenye hisa na maisha hata uwe mjanja kiasi gani maisha bado yanakusomea ramani hivyo kuwa makini acha kukurupuka jipange fanya mambo yako kwa umakini wa hali ya juu kila kitu kwako kitakuwa sawa kwa manufaa yako na jamii kwa ujumla.

Malengo ambayo ni sawa na ilani yako usiyapuuze hata kidogo kwani adui wa kwanza katika maisha ni nafsi yako mwenyewe,ndio ni nafsi yako mwenyewe hebu jiulize swli hili ni mara  ngapi umeiambia nafsi yako kuwa utafanya jambo flani labda kama ni kuacha pombe au kwa mwanafunzi kusoma sana baada ya kufeli mwisho wa siku kila kitu kinabaki vile vile kikielea bila utendaji wowote je katika hili nani ni adui?

Yote kwa yote kuna changamoto kubwa sana katika gharama za maisha kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali ya gharama za maisha na uchumi vinazidi kupanda bila kujua chanzo ni nini na kitu cha kushangaza tunapewa ripoti kwa namba kuwa eti uchumi wa taifa umepanda kwa asilimia hapo ndipo nakumbuka kauli ya mwanaharakati inayosema yani we acha tu,haya ndo maisha yaliyojaa visa na mikasa maumivu na furaha pia.

Tabia za watu huwezi kuzitabiri hata kidogo katika safari ya maisha kwani Yule unayemwamini na kumthamini huenda haitambui thamani yako hata chembe ila yupo nawe kwa sababu unanguvu katika kusukuma gurudumu la maisha lengo lake akifika sehemu anayokusudia aendelee na safari yake bila uwepo wako inaleta huzuni na simanzi pia kwani kumuamini mtu ni sawa na kuwekeza ili baadaye muweze kupata faida pamoja.

Hata uwe komandoo katika hilo lzima litkugusa na kukupa wakati mgumu pia hauna jinsi kwani tumekwisha kutambua kuwa maisha hayana shida na wewe kwa kuwa uliyakuta hata ukiondo tukikusindikiza tutaumia tukirejea tushakusahau na tunaendelea kuparaganyika na harakati zetu pamoja na zile ulizoziacha pia tutaziendeleza kwa kuwa nasi maisha hayana shida na sisi tuliyakuta pia.
Hali ya kukata tama mapema na kuhisi kuwa hakuna njia nyingine ya kufanya ili uweze kufanikiwa huo ni uvivu wa kufikiria ndio maana siri nyingi zilizowekwa kwenye vitabu bado ni gumzo kwa mwanaharakati hajapata muda wa kuzisoma bado anaendelea na harakati za kutafuta maisha kasha baadaye akapunguze mawazo sijui ni mawazo gani hayo yanayopunguzwa kwa mtindo huu wa kisasa kabisa.

Zama za mababu zetu mawazo yalipunguzwa kwa mtindo wa kipekee mathalani kwa mtoto wa kikulima akiwa na mawazo anachofikiria daima huwa ni kulima tu hivyo akipata hilo wazo ataelekea shambani na kulianda shamba kama si msimu wa kulima na kuanza kulima kama ni msimu wa kulima,Wamasai wao wnawaza kuwinda tu ili kuonesha ushupavu na uhodari wakianza kuwaza tu hao porini kuwinda samba ,cha ajabu karne hii kila anayewaza utaskia nataka chupa bora umpe maji ili kushusha presha.

Hakuna tunzo katika kusababisha maumivu kwa mtu mwingine zaidi ya nafsi yako kukusuta ila maisha hayahitaji kulipza kisasi wala kuwa na kinyongo na mtu mwaingine kwani kila mtu anatembea na funguo za mafanikio za mtu asiyemjua watakutana wpi na lini ili aweze kumpa hiyo funguo yake ya mafanikio yatupasa kuwa na upendo kwa wote ili tuweze kufikia malengo na kuwa wanaharakati wa kujitegemea na sio tegemezi.

Yoyote anayekaribishwa na kuingia katika harakati ni sawa na mtu aliyewekwa katika chumba chenye giza na hatambui sehemu ilipo tochi au kiberiti ili aweze kuwasha na kupata mwanga hata apige yowe namna gani giza halitaondoka kwa kuwa hakuna kitendo kinachofanyika zaidi ya kuwa na wazo tu la kuhitaji mwanga maisha yanahitaji wazo na kitendo pia ili kile unachokifikiria kiweze kutokea.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad