Mkopo si rafiki wa maendeleo - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 1 November 2016

Mkopo si rafiki wa maendeleo



WANANCHI wameshauriwa kuweka akiba ili waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea kama kujenga na kusomesha na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima pamoja na kutokuwa na tabia ya kupenda kukopa ili kuimarisha kipato na uchumi.

Afisa Masoko  na uhusiano wa UTT AMIS Rashim Mwanga akitoa huduma kwa mteja

Hayo yamesemwa  Rahim Mwanga Afisa masoko na uhusiano wa UTT AMIS (Taasisi ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha) iliyopo mtaa wa Sokoine na Ohio Dar es Salaam
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Kibaha mkoani Pwani

“Hatushauri wananchi kukopa ila tunawashauri kutafuta mitaji ili waweze kupata faida zaidi kwani mikopo ikizidi inaleta umaskini na kama wanahitaji mikopo,mkopo mzuri ni ule unaowekezwa katika uzalishaji ili upate fedha za kulipa huo mkopo”alisisitiza Mwanga.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa kwa mwananchi yoyote anayayetaka kuwekeza sehemu yoyote ile ni vema kutafuta ufahamu na ushauri kutoka kwa wataalamu  juu ya masuala ya uwekezaji ila maamuzi yanabaki kwa mwananchi mwenyewe.

“Watumieni wataalamu wa masuala ya uwekezaji ili kujua kama sehemu utakayowekeza utapata faida au hasara kwani hakuna mwekezaji anayefikiria kupata hasara hivyo ni muhimu kutafuta ushauri kwani ni bure kabisa” alisema.


Naye Afisa masoko wa UTT AMIS Waziri Ramadhan amewataka wananchi kuitumia taasisi hii kama kiunganishi katika uwekezaji ili waweze kutimiza malengo yao kwani mfuko huo unamjali kila mmoja bila kuwa na ubaguzi wowote ule.

UTT AMIS iliazishwa mwaka 2008  inasimamia mifuko zaidi ya mitano mpaka sasa ambayo ni pamoja na mfuko wa umoja,wekeza maisha,mfuko wa watoto,mfuko wa kujikimu na ukwasi  na ni kwa watu wote.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad