KIMYA kilitawala kwa muda usiopungua dakika tatu mara baada
ya kutokea sauti ya kishindo kikubwa kutoka maeneo yaliyo karibu kabisa na
makazi ya watu hali iliyofanya kila mmoja kuacha shughuli aliyokuwa akiifanya.
| Mazingira yetu tuyatunze na kuyalinda pia |
Wote wakawa wanajiuliza nini hicho kwanini iwe hivyo na
mwanzilishi wa haya mambo ni nani maswali yote yalitoka bila kuwa na majibu
sahihi kwa muda ule kwa wana jamii katika maeneo ya mtaa wa saba .
Nisizame ndo ikawa sauti ya kwanza kuweza kusikika na kusema
kwa nguvu kuwa mambo yanazidi kuwa magumu ,kutahamaki kila mmoja anashika njia
yake baada ya kusikia mlio wa king’ora cha
gari ya polisi kikielekea eneo la
tukio.
Kila mmoja ana uhitaji mkubwa kuishi katika mazingira mazuri
na kuwa na vitu vizuri vynye thamani zaidi ya mwenzake namna ya kuipata na
kumiliki hivyo ndipo kunakuwa na utata mkubwa kwa wale wanaoishi kwenye
mazingira kutumia.
Njia iliyo rafiki kabisa ni kuhakikisha kuwa hakuna
anayepoteza muda na nguvu kuwekeza na kufanya jambo litakalomuumiza yeye na
familia yake pia kwa ujumla umakini unahitajika katika kutekeleza majukumu ya
kujenga taifa.
Mazingira yetu ambayo tunaishi yana mambo mengi na shughuli
nyingi zinazofanyika zinategemea uwepo
wa mazingira ili kufanikisha mipango ya binadamu walio chini ya sayari ya
sayari ya tatu ambayo ni dunia
Kila siku miti inakatwa na hakuna anayejali kuhusiana na
uwepo wa misitu hiyo wala kushughulika na kufuatilia masuala ya upandaji wa
miti baada ya kukata miti katika maeneo mbali mbali nchini yenye hifadhi ya
misitu.
Kuna haja ya kutunza mazingira yetu kwa kuhakikisha kuwa
taratibu na sheria zinafuatwa kwa watu wote kwa kuwa kila kiumbe kinategemea
kuishi na kufanya mipango yote kwenye mazingira tunayoishi.
Aidha serikali iweke mipango rafiki kwa wananchi wake ili
kuweza kuwa ni shirikishi kwa wtu wake na kuhakikisha kuwa ukataji wa miti
kiholela na utupwaji wa taka maeneo yasiyo rasmi unathibitiwa pamoja na kuweka
sehemu maalumu za kutupia taka.
Mazingira yakitunzwa vema yanaleta raha na faraja kwa wale
wanayoyaona na pia kwa manufaa ya kizazi kijacho ambacho nacho kinahitaji
kujengewa mazingira mazuri zaidi kwa kuwa hakuna anayependa kuishi kwenye
mazingira yasiyo na mvuto.
No comments:
Post a Comment