Waandishi wa habari wafundwa - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 1 November 2016

Waandishi wa habari wafundwa

                                           
MTANGAZAJI wa  luniga ya  clouds katika kipindi cha 360 Samweli Nathanaeli amewataka waandishi wa habari kutokukata tamaa mapema katika kupambana na harakati za kutafuta  ajira pamoja na changamoto zinazotokana na maendeleo ya sayansi na technolojia.

Nathanaeli amesema kuwa tasnia ina mambo mengi hivyo kuna umuhimu wa wanahabari kuwa na uvumilivu na kujituma kwa juhudi ili na kuwa wabunifu zaidi kwa kuendana na technolojia na jambo la muhimu kwa waandishi ni kutumikia kwa wanajamii.

Nathaniel Smweli akiwafunda wanahabari waliohudhuria semina iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi Basata
“Uwepo wa mitandao ya kijamii kama facebook , istagrasm ,twiter unafanya wana jamii kuwa na imani zaidi kwa mitandao ya kijamii na tukio lolote likitokea kila mmoja anafanya kazi ya kuripoti
matukio kama mwandishi wa habari”. Amesema

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa mwandishi anajukumu la kujikubali mwenyewe na asihisi kuwa hana uwezo wa kufanya vizuri katika tasnia ya habari na mazingira yasiwe chanzo cha kushindwa kufanya vizuri zaidi.

“Kuna umuhimu wa kujikubali na kujituma kwa kufanya kazi na sio kujikatisha tamaa na kuhakikisha unaweza kufanya mambo kwa mpangilio na kuwa kiraka kwa kuweza kufanya kazi zaidi ya moja katika tasnia ya uandishi na utangazaji pia”.Amesema

Zainabu Nassoro ambaye ni mwandishi wa habari amesema kuwa kuna umuhimu wa kujituma na kupambana na changamoto za maendeleo ya technolojia kwa kuwa ni kitu kisichoweza kuzuilika kirahisi.

“Hakuna anayeweza kuzuia maendeleo ya teknolojia hivyo kuna haja ya kutambua ni namna gani tunaweza kuzishinda na kuendelea kuwa bora zaidi katika kazi yetu ya kufikisha taarifa kwa jamii inayotuzunguka”.Amesema





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad