CHINI ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery kikosi cha KMC kimepita
kwenye dakika 630 za mateso kwa kukwama kusepana pointi tatu zaidi ya katika
mechi 7 mfululizo.
Mechi moja pekee KMC iliambulia pointi moja kwenye sare ya
kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar huku mechi tano wakiambulia kichapo
mazima.
Kwenye msako wa pointi 21 ni pointi moja wamesepa nayo huku 20
zikiyeyuka jumjumla na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao manne huku ile
ya ulinzi ikitunguliwa mabao 11.
Timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni mara ya mwisho kupata
ushindi ilikuwa ni Desemba 22,2022 iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Polisi
Tanzania.
Kete zilizofuata zilikuwa ngumu kwa KMC ambapo ilishuhudia ubao
ukisoma KMC 1-3 Simba, Desemba 26,2022,Ihefu 1-0 KMC, Januari 3,2023,Mtibwa
Sugar 1-1 KMC, Januari 13,2023.
KMC 1-3 Namungo, Januari 24,2023,Ruvu Shooting 2-1 KMC, Februari
5,KMC 0-1 Yanga Februari 22 na Azam FC 1-0 KMC Februari 25.
Kibindoni imekusanya pointi 23 baada ya kucheza mechi 24 huku
vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 62 baada ya kucheza jumla ya mechi 23.
Thiery ameliambia Championi Jumatatu kuwa wanahitaji kupata
matokeo mazuri jambo ambalo wanalipambania na inawezekana kuwa hivyo kwa mechi
zijazo.
“Hakuna anayependa kupata matokeo mabaya kwa mechi zetu za hivi
karibuni zote zilikuwa ni ngumu ninawapongeza wachezaji wanazidi kuwa imara
hivyo kwa mechi zijazo nina amini tutafanya vizuri,”.
No comments:
Post a Comment