WAKATI leo Ihefu wakitarajiwa kumenyana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili rekodi zinaonyesha kuwa vigogo wengi wa Dar wamebuma kusepa na pointi tatu.
Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu,
John Simkoko na Zuberi Katwila ambaye ni msaidizi imekuwa na mwendo bora kwa
mechi wanazocheza nyumbani.
Yanga wao kete yao ya kutofungwa
mechi 50 ilibuma hapo baada ya ubao kusoma Ihefu 2-1 Yanga ilikuwa ni Novemba
29,2023.
Hivyo Yanga walikwama kuendeleza
rekodi ya kutofungwa kwenye mechi za ligi baada ya kucheza mechi 49 mfululizo
bila kufungwa.
Matumaini ya Azam FC kutwaa taji la
ligi yalizimikia kwenye uwanja huo baada ya ubao kusoma Ihefu 1-0 Azam ilikuwa
ni Machi 13,2023.
Simba leo wana kibarua cha kusaka
pointi tatu kwenye Uwanja wa Highland Estate ambao una rekodi ya kutibua mwendo
kwa vigogo hivyo dakika 90 zitaamua kama rekodi itavunjwa na Simba ama rekodi
itaendelea kwa timu kutoka Simba.
No comments:
Post a Comment