INATOSHA kwa maumivu ambayo mashabiki wameyapata pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo ilikuwa ikipambana kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON).
Kwenye mechi tatu ilizocheza ilikuwa ni ngumu kupata tabasamu
kutokana na mechi zote kutoapa ushindi hivyo Watanzania wapo kwenye huzuni ya
kuona kwamba kwa mara nyingine tena tunakuwa ni wasindikzaji kwenye mashindano
haya makubwa.
Kuondolewa kwenye hatua za makundi mara kwa mara inamaanisha
kwamba kuna mambo yanatakiwa kufanyiwa kazi kuanzia kwa wachezaji pamoja na
uwekezaji kuwa mkubwa kwa mipango ya baadaye.
Hatua moja inapofika mwisho haina maana kwamba ni mwisho wenyewe
bali ni mwanzo wa yale yanayokuja ukizingatia kwamba kuna mashindano mengine
mbele.
Hongereni wachezaji kwa namna ambavyo mlijituma kutimiza
majukumu yenu kwa wakati licha ya matokeo kutokuwa rafiki ni sehemu ya mchezo
na mpira una maajabu yake.
Kucheza na timu kubwa inamaana kwamba nanyi kuna hatua ambayo
mnatakiwa muwe hapo na kwa kufanyia kazi makosa wakati ujao mtakuwa imara na
kutoishia kwa mara nyingine hatua ya makundi.
Benchi la ufundi limefanya kazi kubwa kuona namna gani kila
mchezaji anapata nafasi kuonyesha uwezo wake lakini kilichotokea hakiwezi
kubadili matokeo ni hayohayo muda wote.
Wakati ujao ni muhimu kufanya maandalizi mazuri ili kuwapa
furaha mashabiki na wachezaji kutimiza malengo ya kuondoka katika hatua ya
makundi mpaka 16 bora hili sio jambo la haraka mipango lazima ianze sasa.
|
ReplyForward Add reaction |
No comments:
Post a Comment