WABABE wawili walikuwa kazini kwenye msako wa atakayetinga hatua ya fainali ya Mapinduzi 2024 na mwisho mbivu na mbichi zikajulikana ilikuwa Januari 11 2024.
Ni Singida Fountain Gate hawa wanagotea katika hatua ya nusu fainali wakipoteza mechi zote mbili walizokutana na Simba kwenye Mapinduzi 2024.
Walianza hatua ya makundi ubao uliposoma Simba 2-0 Singida Fountain Gate na nusu fainali ilikuwa Singida Fountain Gate 1-1 Simba mshindi kwa penalti Singida Fountain Gate 2-3 Simba.
Fainali inatarajiwa kuwa Mlandege v Simba, Januari 13, hapa tunakueltea baadhi ya kazi ilivyokuwa nzito namna hii:-
Kadi za njano
Ilikuwa ni kazi kubwa kwenye kukaba na kuzuia wa kila mchezaji ambapo miongoni mwa wachezaji walioonyeshwa kadi za njano kwenye mchezo huo ni beki wa kupanda na kushuka Gadiel Michael.
Ilikuwa ni dakika ya 44 alipomchezea faulo kiungo wa kazi Simba, Saido Ntibanzokiza. Mwingine ni Abdulmajid Mangalo yeye alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 50.
Kocha msaidizi wa Singida Fountain Gate alikutana na balaa la kadi ya njano dakika ya 83 akaogezewa nyingine ya pili iliyofanya aonyeshwe kadi nyekundu kwenye mchezo huo wa nusu fainali.
Mapigo huru
Kwa Singida Fountain Gate nyota Marcus Tchakei alipewa kazi ya kupiga mapigo huru upande wa kona alifaya hivyo dakika ya 22, 25 na 45 pia huku kwa Simba kazi hiyo ilikuwa kwenye miguu ya Saido Ntibanzokiza.
Ntibanzokiza alipiga kona dakika ya 90+8 iliyoleta bao kwa upande wa Simba jioni. Pia alikuwa ni nyota aliyechezewa faulo dakika ya 19, 26, 42, 44, 45.
Pia Israel Mwenda alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 27, Shomari Kapombe alipiga faulo dakika ya 45.
Makipa kazini
Ally Salim alikuwa kipa wa kwanza kutunguliwa ilikuwa dakika ya 11 na mtupiaji alikuwa ni Elvis Rupia aliyewapa Singida Fountain Gate bao la kuongoza. Aliokoa hatari dakika ya 59, 63.
Kwenye mapigo ya penalti aliokoa penati tatu ilikuwa ya Gadiel Michael, Hamad Wazir na Meddie Kagere.
Ibrahim Rashid, (Parapanda) dakika 45 za mwanzo ilikuwa lango salama kwake na dakika ya 90+8 alitunguliwa bao na Fabrince Ngoma.
Aliokoa hatari dakika ya 27, 43 kwenye mchezo huo na kwenye mapigo ya penalti aliokoa penalti moja iliyopigwa na Shomari Kapombe huku ile ya Ntibanzokiza ikigonga mwamba.
Bao la usiku
Nyota wa Simba Ngoma alidhihirisha kuwa haijaisha mpaka iishe, wakati Singida Fountain Gate wakiamini kazi imegota mwisho, pigo lake la dakika ya 90+8 lilizama mazima nyavuni na kufanya ubao usoma Singida Fountain Gate 1-1 Simba. Mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penalti.
Kagere gumzo
Mshambuliaji Meddie Kagere kwenye mchezo wa nusu fainali alizua gumzo kutokana na hesabu zake za pigo lake la penalti kugotea kwenye mikono ya Ally Salim. Kagere aliingia uwanjani dakika ya 72 akichukua nafasi ya Rupia.
Mtindo wake wa kupiga penalti ni yeye mwenyewe anajua alichokuwa akifikiria na mwisho alionekana akijutia kile alichokifanya.
Sarri ngoma nzito
Ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba, Babacar Sarr bado ngoma ni nzito kwake kwa kuwa alikomba dakika 60 na nafasi yake ilichukuliwa na Luis Miquissone akimuacha Ngoma akiendelea kutawala kwenye eneo la kiungo mkabaji.
Kenned Juma beki wa Simba ambaye alijichanganya kwenye kuokoa hatari dakika ya 11 kabla ya mpira kuzamishwa nyavuni naye aligotea dakika 45 nafasi yake ikachukuliwa na Hussein Kazi aliyekwenda kupiga kazi.
No comments:
Post a Comment