NGOMA ilipigwa na mwisho wa siku timu nane zimetinga hatua ya
robo fainali Kombe la Azam Sports Federation.
Hapa tunakuletea namna kazi
ilivyokuwa kwa wapambanaji hao kusaka ushindi namna hii:-
Simba 4-0 African Sports, Uwanja wa Uhuru
Ilikuwa Machi 2,2023 ambapo mabao ya Simba yalifungwa na Jean
Baleke dakika ya 36,Kennedy Juma dakika ya 47, Mohamed Mussa dakika ya 69 na
Jimsony Mwinuke dakika ya 90.
Katika mchezo huu Moses Phiri aliweka rekodi ya kutoa pasi mbili
za mabao ilikuwa dakika ya 47 na 90 huku nyota watatu ambao ni Peter Banda,
Mwinuke na Mussa walikuwa super sub.
Mwinuke na Mussa hawa walifunga wakitokea benchi huku Banda yeye
akitoa pasi moja ya bao
Yanga 4-1 Tanzania Prisons
Moja ya mchezo bora uliokuwa na ushindani mkubwa huu unaingia
kwenye orodha kutokana na kasi ya kila timu kusaka ushindi.
Dakika 45 hakuna timu iliyoona lango la mpinzani na mabao yote
matano yalifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo.
Ilikuwa ni Machi 3. Mabao ya Yanga yalifungwa na Bakari
Mwamnyeto dakika ya 52,Clement Mzize alitupia mawili dakika ya 70 na 88 na moja
mali ya Aziz KI ambaye alipachika bao dakika ya 84 kwa mkwaju wa penalti.
Ni Jumanne Elifadhil huyu alipachika bao kwa upande wa Tanzania
Prisons ambalo lilikuwa la kuvutia machozi.
Singida Big Stars 1-0 JKT Tanzania
Matumaini ya wengi yakiwa yameanza kuyeyuka kwa mashabiki wa Singida
Big Stars kutinga hatua ya robo fainali ndani ya dakika 90 mkombozi akatokea
ghafla.
Ni Biemes Carmo huyu alitupia bao jioni dakika ya 90 na
kuwanyanyua mashabiki kwa shangwe na timu hiyo yenye maskani yake Singida
kukata tiketi ya kutinga robo fainali.Ilikuwa ni Machi 3, Uwanja wa Liti.
Geita Gold 3-1 Green Warriors
Vijana wa Felix Minziro walionesha ubabe wao mbele ya wajeda,
Green Warriors ambao walikuwa Uwanja wa Nyankumbu.
Inaungana na timu nyingine kwenye hatua ya robo fainali baada ya
kupenya kwenye 16 bora ilikuwa Machi 3.
Ihefu 2-0 Pan African
Hawana jambo dogo Ihefu wakiwa kwenye ngome yao pale Highland
Estate walipenya hatua ya robo fainai kwa kuitungua Pan African.
Ni Andrew Simchimba alipachika mabao yote mawili na kuizamisha
meli ya Pan ilikuwa dakika ya 23 na 47 ilikuwa Machi 4.
Azam 2-0 Mapinduzi
Azam FC imetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi dhidi ya
Mapinduzi Uwanja wa Azam Complex.
Mtibwa Sugar 1-0 KMC
Msumari mmoja wa David Kameta, ‘Duchu’ dakika ya 45 kwa mkwaju
wa penalti uliwafungashia virago KMC kwenye mashindano haya ilikuwa ni Machi
4,Uwanja wa Manungu.
Kagera Sugar 0-1 Mbeya City
Wakiwa nyumbani Kagera Sugar pale Uwanja wa Kaitaba mambo
yalikuwa magumu kwao baada ya kutunguliwa na Richardson Ng’ondya
Nyekundu zilitembea
Ibraham Abraham beki wa Tanzania Prisons kwenye hatua ya 16 bora
anaingia kwenye orodha ya nyota ambao walionyeshwa kadi nyekundu.
Huyu alionyeshwa kadi mbili za njano na kupelekea kuonyeshwa
kadi nyekundu dakika ya 45 na mwamuzi wa kati. Kadi ya kwanza ya njano
alionyeshwa dakika ya 33 alimchezea faulo Jesus Moloko na ile ya pili dakika ya
44 alimchezea faulo Tuisila Kisinda.
Chalamanda
Ramadhan Chalamanda nyota wa Kagera Sugar ambaye ni kipa huyu
alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mchezo dhidi ya Mbeya City.
No comments:
Post a Comment