ILIKUWA roho ya mnyama kwenye ardhi ya Bongo wakati wakipambana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca.
Weka kando kutokuwepo kwa kipa namba moja Aishi Manula kutokana
na kutokuwa fiti bado ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-0 Wydad
Casablanca.
Kazi haijaisha ugenini hatma ya Simba itajulikana ila hapa
tunakudondoshea namna wapambanaji walivyokuwa kwenye kazikazi namna hii:-
Ally Salim
Aliokoa hatari dakika ya 9,22,23,27,39,57,87,90 alipiga pasi
ndefu dakika ya 3,33,77 zile pasi fupi ilikuwa dakika ya 20,57,87.
Shomari
Shomari Kapombe alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya
69 alipewa majukumua kurusha dakika ya kwanza 7,37,54 huku akiokoa hatari
dakika ya 16,48,59,78.
Joash Onyango
Kakamilisha dakika 90 bila kusababisha penalti katika mchezo
dhidi ya Wydad na alivuja jasho akiokoa hatari dakika ya 23,38,58,67,87 na
alionyeshwa kadi moja ya njano.
Inonga
Henock Inonga aliokoa hatari dakika ya 2,15,23,53,60,72,73
alipga faulo dakika ya 11,
Mohamed Hussein Zimbwe Jr
Aliokoa hatari dakika ya 49 alipiga krosi dakika ya 19,79
alipewa jukumu la kurusha dakika ya 38,64.
Kibu
Kibu Dennis kiungo wa Simba alichezewa faulo dakika ya kwanza,
3,10,18,83 alicheza faulo dakika ya 8,17 alipiga mashuti ambayo hayakulenga
lango dakika ya 34,74 aliokoa hatari dakika ya 49.
Mzamiru
Mzamiru Yassin alichezewa faulo dakika ya 51 alirusha dakika ya
73 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 14.
Chama
Clatous Chama alicheza faulo dakika ya 42,90, alipiga faulo
dakika ya 3,29 alipiga kona dakika ya 35 alipiga shuti ambalo halikulenga lango
dakika ya 46.
Kanoute
Sadio Kanoute kiungo mkabaji wa Simba karejea uwanjani na kusepa
na dakika zote 90 ni dakika ya 26 aliokoa hatari huku akitembeza mikato yake ya
kimyakimya dakika ya 12 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya
31,38 alitembezewa mikato dakika ya 65,71.
Ntibanzokiza
Saido Ntibanzokiza alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango
dakika ya 5,58,alipiga krosi dakika ya 37 alirusha dakika ya 7,alichezewa faulo
dakika ya 65,71 licheza faulo dakika ya 12 alisepa na dakika 80 nafasi yake
aliingia Pape Sakho aliyechezewa faulo dakika ya 82.
Baleke
Jean Baleke aliyeyusha dakika 88 nafasi yake alichukua nahodha
John Bocco alifunga dakika ya 30 alichezewa faulo dakika ya 29,46,62.
Youssef El Motie
Alianza langoni na alitunguliwa bao moja huku akiokoa hatari
dakika ya 55,67,79 alipiga pasi ndefu dakika ya
19,34,36,38,52,55,67,69,71,75,76.
Jamal Daoudi
Nyota huyu alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 52 aliokoa hatari
dakika ya 65.
Abduolatif
Aliokoa hatari dakika 7 alionyeshwa kadi moja ya njano.
Asen Zola
Mwamba huyu alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 16
huku akiokoa dakika ya 18,20,64,84 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86.
Yahya Abdalah
Aliokoa hatari dakika ya 48,60 alicheza faulo dakika ya 45
alipiga kona dakika ya 23,38,48.
No comments:
Post a Comment