SIO utani kwenye kusaka ushindi kimataifa kazi ni ngumu ndani ya dakika zote 180 licha ya kuwa kila timu kufanya maandalizi mazuri.
Uwanja
wa Mkapa, Simba walianza kazi yao kwa kupata ushindi dhidi ya Wydad Casablanca
kisha mchezo unaofuata utakuwa ugenini.
Hakika
kwa ushindi wa mchezo wa kwanza Simba mnapaswa pongezi huku mkitambua kuwa mna
kazi ugenini.
Haitakuwa
kazi nyepesi bali ni ngumu kwa kila timu kupata ushindi kutokana na maandalizi
na uhitaji wa kila timu kupata ushindi.
Makosa
ambayo yamefanyika kwenye mchezo wa kwanza ni muhimu kufanyia kazi huku
wachezaji wakiongeza umakini kwenye mchezo wa kukamilisha robo fainali ya pili
ugenini.
Kikubwa
ni kufanya jitihada kwenye dakika 90 zilizobaki kwenye anga za kimataifa ili
kufungua ukurasa wa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
Mida
ya malisho kwa wachezaji ni sasa katika kufanya maandalizi ya mwisho kwa kuwa
kila mmoja ana kazi yake kwenye kusaka ushindi.
Yanga
kete ya ugenini ambayo ilitarajiwa kukamilishwa jana ni mwanzo wa kusaka ngwe
ya pili kusaka hatua ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.
Wale ambao watakuwa mbali ya Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa marudio waendeleze dua kwa ajili ya Yanga kupata ushindi na wale ambao watakuwa karibu ni muda wao kujitokeza kuishangilia timu kwa shangwe.
Ushindi ambao wameupata ugenini ni muhimu kuendelea kuulinda kwenye mechi ya pili kukamilisha hesabu za kutinga hatua ya nusu fainali.
Wachezaji
kazi ni kwenu kwa kuwa muda uliobaki hautoshi kupoteza ziadi ya kutumia kwa
umakini katika kusaka ushindi na inawezekana.
No comments:
Post a Comment