NDANI ya KMC yenye maskani yake Kinondoni panga kubwa linatarajiwa kupita kwa mastaa wao ili kuunda kikosi kipya cha ushindani.
Timu hiyo imebaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa ushindi kwenye mchezo wa mtoano KMC imewaandikia mastaa 11 barua za kuwapa mkono wa asante.
KMC ilibaki ndani ya ligi kwa ushindi wa jumla ya
mabao 3-2 Mbeya City ambayo hii itashiriki Championship.
Mbeya City kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa
Sokoine ilipata ushindi wa mabao 2-1 na mchezo wa pili wa kumsaka mshindi
ikashuhudia ubao wa Uwanja wa Uhuru ukisoma KMC 2-0 Mbeya City.
Hivyo ni rasmi kuwa KMC bado wapo ndani ya ligi na
wanatarajia kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi hicho.
Ni wachezaji 11
wanatarajiwa kupewa mkono wa asante kwa ajili ya kuwapa nafasi nyota wengine
wapya kwenye kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment