SAINI BORA NDANI YA YANGA KUTOKA KWA MWAMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 13 July 2023

SAINI BORA NDANI YA YANGA KUTOKA KWA MWAMBA


 

AMONG of the Quality sign hivyo tu basi unaweza kusema ikiwa utahitaji kueleza kuhusu usajili wa Yanga kwa kiungo wa kazi eneo la kati anayeitwa Jonas Mkude.

Ni yeye Jonas Mkude hivi karibuni alipokuwa akizungumzia kuhusu yeye kuibuka ndani ya Yanga tetesi zilipokuwa nyingi hakuzungumza maneno mengi wala machache lakini yalikuwa na uzito mkubwa sana.

Mkude alikutana na Thank You ndani ya Simba na ilikuwa ni ganzi kwa mashabiki hata yeye mwenyewe alikiri kuwa hakujua kama ingekuwa hivyo lakini maisha ya mpira lazima yaendelee kwa kuwa mkataba wake ulikuwa umegota mwisho

Juni 22 alikutana na Thank You Mkude akiwa mchezaji huru huku Simba wakibainisha kuwa muda umewatenganisha Simba na Mkude hivyo hawana namna lazima maisha yaendelee kwa kila mmoja kupambania kombe.

Tukirudi kwenye jibu ambalo Mkude alijibu baada ya kuulizwa kuwa kama ataibukia ndani ya Yanga akitokea Simba ni yeye kwa upole na nidhamu kubwa alibainisha namna hii:" Tuombe Mungu".

Jibu moja fupi lenye maana kubwa zaidi ya ukubwa wenyewe na maombi yamejibu kwa kuwa Mungu ni wetu sote na Mkude maombi yake yamejibu hatimaye ametambulishwa ndani ya Yanga.

Julai 12 2023 itakuwa kwenye vitabu vya kumbukumbu vya Wanasimba na wale wa Yanga kuipata saini ya mzawa mwenye kipaji eneo la kati akiacha yale makando yake ambayo alikuwa anakutwa nayo ndani ya Simba hasa kwenye upande wa nidhamu.

Wanasema ni mkataba wa mwaka mmoja kasaini una kipengele cha kuongeza mwaka mwingine ikiwa ataonyesha uwezo wote mkubwa pamoja na kutimiza majukumu yake, hivyo tu basi.

Mkude kwenda Yanga ni moja ya usajili mzuri na hivi karibuni Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga aliweka wazi kuwa walichokifanya watani zao wa jadi watajutia.

"Ikiwa kuna mambo ambayo watajutia watani zetu wa jadi ni kumpa Thank You Mkude, moja ya wachezaji wazuri kwenye eneo la kiungo.

"Tukiipata saini yake nitawaambia Waananchi tumempata mchezaji mzuri,".

Wananchi wamepata walichokuwa wanakihitaji huku Kamwe akiwa amepata maneno ya kuanza kusema kwa kuwa aliwaahidi Wananchi atarudi na kuwaambia, "Wananchi Tumepata Mchezaji Mzuri'.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad