MAABARA ya Taifa ya Tanzania leo Julai 14 imehitimisha mafunzo ya wataalamu wa afya kutoka nchi 14 za Afrika ambayo ni mafunzo ya ulinzi na usalama wa kibaiolojia.
Nchi ambazo zimeshiriki ni pamoja na Tanzania, Rwanda, Madagascar, Uganda, Morocco, Ushelisheli, Kenya, Burundi kwenye mafunzo hayo ambapo washiriki walipata fursa ya kupata vyeti vya ushiriki na kufanya mitihani pia.
Dr.Ambele Mwafulango, Meneja wa Maabara ya Taifa ameweka wazi kuwa ni fursa ambayo Tanzania imepata kutoa mafunzo hayo ambayo yamekuwa na mafanikio makubwa.
"Tanzania tumepata fursa ya kutoa mafunzo haya kwa Wataalamu wa afya kutoka kwa mataifa mbalimbali na wao wameonyesha kufurahia mafunzo pamoja na mazingira ya Tanzania.
"Shukrani nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akitoa ushirikiano kwenye kila idara jambo ambalo limefanikisha pia mafunzo haya.
"Kila mshiriki amefurahia haya na tumewaambia kwamba kabla ya kuondoka kuelekea kwenye nchi zao wasisahau kufanya matembezi pia pamoja na kununua vitu kutoka Tanzania ukizingatia hapa bidhaa zake bei kila mmoja anaimudu," amesema Ambele..
No comments:
Post a Comment