WASIO NA TIKETI SIMBA DAY WAPEWA ONYO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 6 August 2023

WASIO NA TIKETI SIMBA DAY WAPEWA ONYO


MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa kwa wale ambao hawana tiketi za Simba Day wanapaswa wasifike maeneo ya Uwanja wa Mkapa.

 Agosti 6 ni kilele cha Simba Day na wale ambao hawajapata tiketi taarifa zimeeleza kuwa tiketi zimeisha.

Hivyo kwa wale ambao walikuwa wanahitaji kushuhudia burudani na utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi msimu wa 2022/23 ikiwa hawajanunua tiketi basi wasifike eneo la tukio.

 Ahmed amesema:"Tunawasisitiza wale wote ambao hawajanunua tiketi kabisa wasisogee eneo la Uwanja wa Benjamin Mkapa. Kama huna tiketi kaa nyumbani Jeshi la Polisi Iinasisitiza ili kupunguza usumbufu usio wa lazima. Ambao hawana tiketi wanaweza kufatilia kupitia Azam TV.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad