KAZI kubwa inaendelea kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2023 kutokana na kilatimu kuonyesha ushindani mkubwa uwanjani.
Ipo wazi kwamba wenyeji Ivory Coast mwendo wameumaliza huku mashabiki wakiwa na hasira kutokana na timu hiyo kushindwa kuwa kwenye ubora ambao walikuwa wakiutarajia mwisho wa sio misha lazima yaendelee.
Kua nyota kibao waliopo ndani ya AFCON ikiwa ni pamoja na Mbwana Samatta, Simon Msuva, Kibu Dennis, hawa ni kutoka Tanzania ambapo ni Msuva pekee katupia bao moja.
Mo Salah haawa kwenye ubora baada ya kupata maumivu huku Victor Osimhen, Sadio Mane, Inaki Williams Nicolas Jackson wakiwa hawapo kwenye orodha ya wakali wa kucheka na nyavu..
Ni Emilio Nsue wa Guinea ya Ikweta ambaye kiasilia anachezea nafasi ya beki wa kulia katika Klabu ya CF Intercity ya Ligi daraja la tatu Uhispania ni kinara akiwa na mabao matano.
Laurent Pokou ndio mchezaji pekee aliyewahi kufunga mabao mengi zaidi (7) kwenye hatua ya makundi ya michuano ya AFCON kumzidi Nsue mwenye mwenye mabao matano.
No comments:
Post a Comment