MRITHI wa mikoba ya mshambuliaji, Jean Baleke ambaye anaondoka akiwa namba moja kwenye utupiaji ndani ya ligi akiwa katupia mabao 8, Michael Fred ana balaa kutokana na rekodi zake.
Ni Michael Fred raia wa
Ivory Coast anatajwa kubeba mikoba ya Baleke ambaye hatakuwa ndani ya kikosi
cha Simba kwa msimu wa 2023/24 kwenye mechi zilizobaki kitaifa na kimataifa.
Baleke anaondoka Simba na
Moses Phiri wote walikuwa kwenye kasi ya ufungaji wa mabao na katika Mapinduzi
2024 wote walifunga bao mojamoja na Simba iligotea nafasi ya pili mabingwa
wakiwa ni Mlandege.
Michael kwenye ligi ya
Zambia kwenye mechi 18 alizocheza alifunga jumla ya mabao 14 huku akitengeneza
pasi nne za mabao.
Rekodi hizo ni balaa ikiwa
zitajibu kwenye mechi za ligi huenda akavunja rekodi ya Baleke aliyefunga mabao
8 msimu wa 2022/23 na msimu wa 2023/24 wakati anakutana na Thank You alitupia
mabao 8.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara
ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua uimara walionao
wachezaji wao hivyo hawana mashaka.
“Kazi kubwa ambayo ipo kwa
washambuliaji wetu wapya ni kufunga mabao tunaamini kwamba wachezaji watatimiza
majukumu yao na tutashangilia mabao,”.
No comments:
Post a Comment