KWENYE ishu ya usajili siyo Bongo tu kwamba wanasajili kwa mikwara mingi mwisho wa siku wachezaji wanabuma hata Ulaya hiyo ipo.
Unakumbuka usajili wa maana uliofanywa na Yanga kwa Michael Sarpong, mwili jumba ila mwisho wa siku akafunga mabao manne kisha akavunjiwa mkataba na kusepa zake kuelekea Ghana?
Weka kando huyo unamkubuka David Molinga, vipi kuhusu Perfect Chikwende yule wa Simba pamoja na Ally Niyonzima wa Azam basi leo tunakuletea baadhi ya nyota ambao walisajiliwa kwenye timu kubwa Ulaya ila mambo yakawa magumu kwao namna hii:-
Timo Werner
Kabla ya kutua Chelsea nyota huyu alikuwa ndani ya kikosi cha RB Leipzig inayoshiriki Bundesliga na alikuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza.
Msimu wa 2019/20 akiwa huko aliweza kutupia jumla ya mabao 34 na pasi za mwisho 13 hapo akawafanya mabosi wengi kumtazama kwa ukaribu na Chelsea ikampata kwa dau la pauni milioni 50 akaingia ndani ya Ligi Kuu England.
Kwa sasa mambo kwake ni magumu hajaonyesha yale makeke katika kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel alifunga jumla ya mabao 12 kwenye michuano yote akiwa na Chelsea msimu uliopita anatajwa kurudi tena Ujerumani huku Bayern Munich wakipewa kipaumbele kusepa na saini yake.
Takumi Minamino
Aliibuka ndani ya Ligi Kuu England kwa mikwara kinoma akitokea Klabu ya RB Salzburg baada ya kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019.
Liverpool hawakuona shida kuweka mezani pauni milioni 8 mwaka 2020 hapo picha jipya likaanza mechi 10 akacheza hakuna ishu ya kufunga wala pasi ya bao mambo yakawa magumu kwake.
Msimu uliopita akapata zali la kucheza mechi tisa za Ligi Kuu England kabla ya kupelekwa kwa mkopo ndani ya Southampton na alishindwa kuwika huko akarudi Liverpool, bado yupoyupo tu na anaweza kusepa muda wowote.
Raheem Sterling
Ninja huyu ni zao la Akademi ya Liverpool, alikuwa na mchango mkubwa alipokuwa hapo na aliweza kuhusika kwenye mabao 39 katika mechi 95 za Ligi Kuu England ndani ya kikosi hicho kisha akapata zali la kujiunga na Manchester City 2015.
Akawaka tena ndani ya City kwenye jumla ya mechi 203 alitupia mabao 79 na pasi 51 ila msimu huu wa 2021/22 mambo yanaonekana kuwa magumu kwake na anaweza kusepa hapo kwa kuwa nafasi yake ni kiduchu sana.
Hakim Ziyech
Jamaa alitua ndani ya Chelsea Julai Mosi 2020 akitokea Ajax kwa dau la pauni milioni 36 huko unaambiwa alitupia mabao 48 na pasi 81.
Ziyech kwa sasa hafurahii maisha yake ndani ya Chelsea ambapo rekodi zinaonyesha kwamba amecheza mechi 16 za Ligi Kuu England huku mchawi akiwa ni majeruhi ya mara kwa mara na anatajwa kwamba atakwenda AC Milan.
Donny Van De Beek
Unaambiwa moja ya kile kizazi cha dhahabu cha Ajax tangu ametua ndani ya Manchester United Septemba 2020 amebuma jumlajumla.
Nyota huyo alikuwa kati ya viungo matata kutoka Uholanzi na alikuwa bora pia kwenye ligi ya huko ila ndani ya United hakuna ambacho kinatokea kwake.
Ni mechi 20 amecheza ndani ya Ligi Kuu England na nne pekee alianza kikosi cha kwanza presha kubwa inatokana na yeye kukaa benchi hivyo mambo yakiwa hivyo tena anaweza kusepa.
No comments:
Post a Comment