Maneno yao ya mwisho kuongea na wachezaji na kufanya dua ya pamoja ilikuwa ni Oktoba 22, Uwanja wa Boko Veteran ambapo walikuwa katika maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao ulibadili upepo Oktoba 24 baada ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 1-3 Jwaneng Galaxy.
Pia waliweza kufanya dua ya mwisho na kupiga stori za hapa na pale huku mashabiki wakiwa wamejitokeza kushuhudia mpango mzima.
Wakati wa kusepa nyota wao Meddie Kagere pamoja na Hassan Dilunga walionekana wakizinguana kimtindo ila mwisho wa siku maisha yaliendelea kama ilivyo ada.
No comments:
Post a Comment