MAKOCHA wapya wa Simba ikiwa ni pamoja na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery alikuwa ndani ya Uwanja wa Mkapa na amesimamia mchezo wa kwanza mbele ya Polisi Tanzania.
Aly Salim kipa namba tatu wa Simba leo alikuwa na jukumu la kuwanoa Aishi Manula na Beno Kakolanya ambao ni makipa wa timu hiyo.
Hii ni baada ya Kocha wa Makipa aliyekuwa akiwanoa Simba Milton Nienov kupigwa chini na kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy
Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 27 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Polisi Tanzania na bao lilipachikwa kwa mkwaju wa penalti na Rarry Bwalya.
No comments:
Post a Comment