PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City ameweka wazi kuwa mchezo ujao ambao ni wa dabi dhidi ya Manchester United ni muhimu kwao kuweza kusepa na pointi tatu muhimu.
Kesho, Novemba 6, City itakuwa ugenini, Uwanja wa Old Trafford kumenyana na United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England akiwa na kumbukumbu ya kutoka kuiongoza timu yake kwenye ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Club Brugge katika mchezo wa Uefa.
Wakati City wakiwa tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho taarifa mbaya kwa mashabiki wa Manchester United ni kuhusu kukosekana kwa beki wao wa kazi Raphael Varane ambaye aliumia nyama za paja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atalanta.
Mbali na mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa pia kesho kutakuwa na mchezo mwingine mkali kati ya Chelsea dhidi ya Burney utakaopigwa Uwanja wa Stamford Bridge saa 12:00.

No comments:
Post a Comment