CRISTIANO Ronaldo mwenye miaka 36 na siku 267 ni moja ya washambuliaji wanaofanya vizuri ndani ya uwanja na sasa yupo zake ndani ya Manchester United.
Amekuwa ni mchezaji ambaye anaingia kwenye rekodi ya kufunga na kutoa pasi ya bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kwa msimu huu wa 2021/22 akiwa na umri huo.
Mara ya mwisho kutokea hivyo ilikuwa ni Didier Drogba ambaye alifanya hivyo mwaka 2014.
Pia wakati huo Drogba alikuwa na miaka 36 na siku 267 na alifanya hivyo mbele ya Spurs kama ilivyokuwa kwa Ronaldo.
Katika mchezo huo Ronaldo alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo na timu yake ilishinda mabao 3-0.

No comments:
Post a Comment