KIKOSI cha Yanga leo Novemba 2 kimesepa na pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Mabao ya ushindi kwa Yanga yalifungwa na kiungo Feisal Salum dk 32 beki Djuma Shaban dk 46 kwa mkwaju wa penalti na Tonombe Mukoko dk 75.
Kwa upande wa Ruvu Shooting bao lilipachikwa na Shaban Msala dk 8 lilikuwa ni bao la mapema na la kwanza kwa kipa Diarra Djugui kuokota nyavuni.
Pia kwenye mchezo wa leo dk 24 Santos Mazengo wa Ruvu Shooting alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Fiston Mayele.
Yanga inajikita kileleni ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi tano ndani ya msimu wa 2021/22.

No comments:
Post a Comment