BEKI wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania,Juma Ramadhan amesema kuwa hana hofu na mshambuliaji yoyote Bongo jambo linalompa nafasi ya kutimiza majukumu yake.
Mkwara huo unawahusu moja kwa moja mastaa wa Simba waliopewa majukumu ya kufunga ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere mwenye mabao 7 na pasi moja pamoja na Bernard Morrison mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.
Ramadhan ambaye ni nahodha aliweka wazi kuwa kwenye kila mechi ambazo wanacheza hesabu zao ni kuzuia hali ya kufungwa pamoja na kusaka ushindi.
“Kwa timu zote hapa ninaona kila kitu ni maandalizi hivyo hakuna mshambuliaji ambaye ananitisha nikipewa nafasi ya kuanza lazima nitatimiz majukumu yangu kwa kuzuia kufungwa.
“Nakumbuka mchezo wetu dhidi ya Simba nilitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu hilo jambo liliniuma kwa kuwa timu yetu ilipoteza hivyo kwa mechi zijazo lazima kazi itafanyika,” amesema Ramadhan.
Nyota huyo ameanza kikosi cha kwanza mechi 6 na ametoa pasi moja ya bao kati ya 14 ambayo yamefungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya 9.
No comments:
Post a Comment