SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa kwa sasa
wanafanyia kazi makossa ya wachezaji wao ikiwa ni pamoja na tatizo la
umaliziaji wa nafasi ambazo wanazipata.
Mabingwa hao watetezi kwenye msimamo wapo nafasi ya pili wakiwa
wameachwa pointi 11 na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 51.
Matola amesema kuwa
wanatambua kwamba kuna makosa ambayo yapo jambo ambalo wanalifanyia kazi kila
wakati.
“Makosa yapo kwenye mechi ambazo tunacheza tunaona kwamba hata
mchezo wetu dhidi ya Coastal Union tuliweza kupoteza nafasi ambaz
tulizitengeneza hivyo hilo tunalifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi,”
alisema.
Wakati Simba ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union wachezaji
wa timu hiyo walikosa nafasi 10 za kufunga ambazo ziliokolewa na kipa wa Coastal
Union, Mussa Mbissa.
No comments:
Post a Comment