SERENGETI GIRLS YAPIGA 4 G KIMATAIFA,KAZI BADO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 23 May 2022

SERENGETI GIRLS YAPIGA 4 G KIMATAIFA,KAZI BADO


 TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Wasichana chini ya miaka 17, Serengeti Girls, jana imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Cameroon kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa mtoano wa kuwania kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Mabao matatu yalifungwa na nyota Clara Luvanga huku moja likijazwa kimiani na Diana William kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Omnisport Ahmadou Ahidjo ulioko Yaounde.

Baada ya mchezo wa jana timu inatarajiwa kurejea Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa,Juni 5 mwaka huu na mshindi wa jumla atafuzu kushiriki Kombe la Dunia nchini India mwaka huu Oktoba.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wilfres Kidao ameweka wazi kwamba licha ya ushindi ambao wameupata bado kazi haijaisha kwa kuwa kuna mchezo mmoja.

"Pongezi wanastahili hasa baada ya kushinda mchezo wa kwanza bado kazi haijaisha mpaka tutakaposhinda mchezo wa pili Dar, hivyo nina amini kwamba benchi la ufundi litafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili kushinda," amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad