MBINU zake zinaanza kuonekana kufeli na hata mwalimu wake huenda kwa sasa hamuambii kuhusu makosa makubwa ya uzembe ambayo amekuwa akifanya.
Inaonekana hana mazungumzo mazuri na safu yake ya ulinzi na hata hesabu zake zinamgomea katika kutimiza majukumu yake hili ni balaa lingine kwa Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa.
Ni mechi nne mfululizo anatunguliwa Air Manula ndani ya kikosi cha Simba akiwa langoni tena mabao ya ajabu kabisa ambayo hata yeye mwenyewe huenda anayashangaa lakini anatunguliwa kwelikweli.
Bao alilotunguliwa na Jeremia Juma limrudishe kwa mara nyingine Manula darasani kwa kuwa ni moja ya bao ambalo hakuwa na chaguo la kufungwa.
Pongezi kwa Juma kwa utulivu mkubwa ndani ya 18 kisha akamtungua Air Manula ambaye hakuwa na chaguo la kufanya.
Katika mchezo huo wa funga mwaka 2022, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 7-1 Tanzania Prisons.
Mchezo uliozalisha mabao mengi kwa msimu wa 2022/23 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Alifungwa mbele ya Kagera Sugar sare ya kufungana bao 1-1 pia alifungwa kutokana na kukwama kuwapanga mabeki wake.
Funga kazi ni bao alilofungwa mwaka 2023 mbele ya Mbeya City dakika ya 78, mpira ulioonekana kutokuwa na hatari akaupuuzia, kwa hatua ambayo amefikia Air Manula ule ni uzembe na anapaswa kuongeza umakini.
Ni bao lake mwenyewe kajifunga na kuiongezea presha Simba na kuonyeshwa kadi ya njano.
Ilikuwa ni siku mbaya kwa wachezaji wote wa Simba kwa kuwa walicheza pira ambalo wanalijua wenyewe na mbinu za kocha wao mpya.
Benchi la ufundi la Simba kwa upande wa makipa lina kazi nzito kuanza kuwanoa makipa wao.
Happy New Year 2023
No comments:
Post a Comment