WAKATI Simba wakitamba kupiga pira Dubai kutokana na kambi yao ya wiki moja waliyoweka huko, vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga wametamba kuwapigia pira popcon wapinzani wao Ruvu Shooting.
Leo Uwanja wa Mkapa, Yanga watawakaribisha Ruvu Shooting kwenye
mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao
2-1 hivyo leo Ruvu watakuwa wanahitaji kuvunja mwiko huyo wakati Yanga
wakipambana kulinda rekodi yao.
Ofisa Habari wa Yanga, Ali
Kamwe amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuwakabili Ruvu Shooting na
watawaigia pira popcorn.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna ambavyo tutakuwa na
kazi kubwa na nzuri kwenye kusaka pointi tatu ambapo tutacheza pira popcorn mbele
ya wapinzani wetu.
“Tumekuwa na rekodi bora kwenye mechi za hivi karibuni jambo
ambalo linatufanya tusiwe na mashaka kwenye mechi tunazocheza kikubwa ni kuzidi
kujenga hali ya kujiamini na kucheza kwa nidhamu,” amesema Kamwe.
Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 53 inakutana na Ruvu
Shooting yenye pointi 14 zote zimecheza mechi 20 msimu huu.
No comments:
Post a Comment