MABADILIKO ya hali ya hewa yamekuwa yakichangiwa kwa kiasi
kikubwa na shughuli za binadamu wenyewe kama vile kilimo,ujenzi wa aina yopyote
pamoja na ufugaji ambao huitaji maeneo makubwa ili kuwekeza hali inayopelekea
kukata miti katika eneo husika.
Katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete ilikuwa
ikitumia sera ya kata mti panda mti lengo kubwa ilikuwa ni kuitoa Tanzania
katika hatari ya kuingia katika jangwa kubwa la ukame na kuweza kuyatunza
mazingira.
Msimamizi wa CBTL Neema Kalenga akitoa ufafanuzi wa mkaa Mkombozi |
Kampeni ilipokewa vizuri kwani Taifa zima lilihamasika na
kuanza kupanda miti katika maeneo mbalimbali waliyokuwa wakiishi na wale
waliokuwa wakikata miti ili kuchoma mkaa nao pia kwa kiasi kikubwa walihusika
kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Wimbo wa kila siku kwa nchi yetu ni kuanza vizuri kabisa
katika mpango na kuishia kati kati bila kujua tulikoanza na tunakoelekea
hali inayofanya tuanze kurejea kulekule tulikotoka muda sio mrefu tena tukajisahau tukaendelea na shughuli zetu sera ikatupwa kule.
hali inayofanya tuanze kurejea kulekule tulikotoka muda sio mrefu tena tukajisahau tukaendelea na shughuli zetu sera ikatupwa kule.
Bado tatizo limekuwa kubwa ukataji wa miti umekuwa
ukiongezeka tena kwa kasi zaidi kadri siku zinavyokwenda na matumizi ya mkaa
yanazidi kupamba moto kwani jiji pekee la Dar es Salaam lenye wakazi wengi ndio
kinara kwa kutumia mkaa cha kufurahisha ni kwamba hakuna msitu maalumu katika
jiji.
Kwa maana hiyo mkaa unaotumika katika jiji la Dar es Salaam
unatoka mikoa ya karibu kama vile Morogoro,Iringa na Tanga huku ndiko misitu
inavunwa na kutengeneza nishati ya mkaa kwa matumizi ya nyumbani.
Baada ya kuligundua hilo kuwa ni tatizo katika bara la
Afrika kiujumla kampuni ya Charcoal
Briquettes Tanzania limited (CBTL) wamekuja na mbinu mbadala kabisa ya kuokoa
mazingira kwa kuyatunza na ukataji holela wa miti kwa kuzalisha mkaa unaoitwa
Mkombozi.
Msimamizi na mtoa mafunzo wa mradi huo Neema Kalenga
anaeleza namna walivyojipanga kuhakikisha kuwa wanaitunza ardhi ya Tanzania kwa
kuiweka katika hali ya usalama zaidi kwa kutumia mbinu mbadala na rafiki wa
mazingira
Ili kuokoa mazingira yetu tumeanza kutengeneza mkaa ambao
hautumii miti katika kuutengeneza hali inayofanya tuokoe miti mingi zaidi na
kutengeneza mkaa bora kabisa kwa kutumia masalia ya taka za shamba katika
kutengeneza mkaa alisema Neema
Tunatengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya shambani kama vile
mabua,nyasi za mpunga,vijiti vidogo vidogo pamoja na maranda ya mbao tunazalisha mkaa safi kabisa na unafaa kwa
matumizi ya nyumbani na kiwandani pia
Lengo letu kubwa ni kuweza kuyatunza mazingira yetu kwa
kuanza na mradi huu na tunatoa elimu kwa wananchi ili waweze kuutambua mkaa huu
na kuutumia kwani haiuna madhara yoyote yale na ni kwa bei nafuu sana
unajipatia mkaa huu aliongeza Neema
Kuhusu mafunzo ya kutengeneza mkaa huo anaeleza kuwa
walipata mafunzochini ya mkurugenzi Nachiket Potnis kutoka India na walianza kufundisha mikoa kama vile
Pwani kisha wakasogea Dar es Saalaam.Tanga na Morogoro lengo likiwa ni moja tu
kutunza mazingira .
Bado watanzania hawajaanza kuuelew mkaa kwani kuna mkaa
mwingi sana katika stoo yetu hali inayotupa wasiwasi kuwa bado mazingira
yanazidi kuharibika na miti inazidi kukatwa nawaomba watanzani waweze
kubadilika na kuanza kutumia nishati rafiki wa mazingira alisisitiza Neema
Tunawafikia watanzania kwa kutumia mawakala wetu waliopo sehemu
mbali mbali na pia kwa njia ya matangazo ili waweze kujua uwepo wetu sisi na
kutumia bidhaa zetu wengi huhisi mkaa huu ni sawa na jiwe hivyo hauwezi kuwaka
wao wanaogopa.
Anafafanua namna unavyotengenezwa kwa kusema mabaki ya mimea
hutengenezwa kuwa vumbi la mkaa kwa kutumia mitambo maalumu ya kutengenezea
mkaa kisha tunasindika mkaa na kuupooza
katika vichanja kwa muda wa siku mbili au tatu tayari kwa matumizi
Wakulima ,wajasiriamali na vijana huwauzia mabaki hayo ya
mimea katika maeneo waliyopo na kuwafanya waweze kuzalisha bidhaa kwa wingi
katika viwanda vyao vilivyopo Bagamoyo na Mlandizi Mkoani Pwani.
Anatoa wito kwa serikali na jamii kuweza kuwaunga mkono
katika juhudi za kutunza mazingira ili kuwa na mazingira bora
yatakayovutia na kufanya tusiweze
kuathirika kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwani Tanzania ni
yetu sote alisisitiza Neema alipokuwa akiongea na gazeti hili.
Naye Diwani wa Kibaha kata ya Mail Moja Ramadhan Lutambi
amewasihi wafanyabiashara kutengeneza bidhaa zenye ubora na kuziuza kwa bei
nzuri ili wasimuumize sana mteja kwani katika mapambano haya kila mmoja lazima
ahusike ipasavyo.
No comments:
Post a Comment