WATANZANIA KUPATA MKWANJA KUPITIA PLAY & WIN - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 27 October 2021

WATANZANIA KUPATA MKWANJA KUPITIA PLAY & WIN


 LEO Oktoba 26, 2021 Kampuni ya Halotel Tanzania kupitia huduma yake ya HaloPesa, inawaletea wateja huduma nyingine bora inayowapa fursa ya kujishindia zawadi kabambe.

 HaloPesa leo imeanzisha kampeni ya "PLAY & WIN" kwa wateja wake wote nchini. HaloPesa inakusudia kuwazawadia wateja wake mamilioni ya fedha na zawadi mbalimbali kila siku, kila wiki na kila mwezi kupitia michezo rahisi na shirikishi ya PLAY & WIN iliyopo katika menyu ya HaloPesa kupitia*150*88#.

 Magesa Wandwi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa HaloPesa alisema:-

"HaloPesa zaidi tu ya kuwa huduma ya kifedha, sasa ni Huduma Jumuishi ya Kifedha na Mtindo wa Maisha kwa wateja wetu. Katika mengi yenye ubunifu ambayo tumewezesha, ni pamoja na kuwapa fursa wateja wetu kuweza kununua muda wa maongezi kwa mitandao mingine. Uzinduzi wa huduma ya PLAY & WIN na Dunia Investment leo, ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka HaloPesa kufikisha thamani hiyo ya mtindo wa maisha kwa wateja wetu wote nchini. ”

 

PLAY & WIN ni ubia wa kimkakati kati ya Dunia Investment & HaloPesa unaowezeshwa na Axieva Africa, kuzindua aina mbalimbali za michezo ya kubahatisha nchini. Michezo hiyo ni pamoja na Tatu Dodo, Bid2Win, Win X-Multiply, Mega 5,000,000 n.k. Wateja wetu waendelee kucheza na Kutumia huduma zetu bora za HaloPesa na wajipatie fursa ya kujishindia Pesa na Zawadi mbalimbali. Aliongeza Magesa.

 

 Kobus Schoeman, Mkuu wa huduma na mahusiano kwa wateja wa Dunia Investment- mbia wa huduma ya PLAY & WIN- amesema:- "Michezo na Burudani ni sehemu asili ya utamaduni wetu wa Kiafrika. Kwa namna moja au nyingine, hakuna siku hata moja ambapo hatuigusi katika Maisha yetu! 


"PLAY & WIN kwa ushirikiano na HaloPesa, inakusudia kuleta utamaduni huo kwenye Simu ya Mkononi. Iwe ni mteja asiye na ujuzi wa michezo ya bahati nasibu na mwenye shauku au mchezaji anayefahamu na kufurahia michezo ya bahati nasibu, PLAY & WIN utakuwa ni mchezo wa wote. Huduma hii pia inajumuisha watumiaji wa aina zote za simu, na lugha ya Kiswahili.

 

"Tuna hakika kwamba, wateja zaidi wa HaloPesa watafurahia huduma ya PLAY & WIN. Na wateja ambao bado hawatumii HaloPesa, watajiunga ili kufurahia faida za huduma hii.”aliongeza Kobus.

 

Kitu kikubwa kwenye Kampeni hii ni HALOPOINTS ZA BURE! Kulingana na aina ya miamala, mteja atapewa HALOPOINTS ZA BURE moja kwa moja wakati wowote anapofanya baadhi ya miamala ya HaloPesa. Kulingana na aina ya muamala, mteja anaweza kupata Halopoints kisha kuzitumia kwenye Michezo ya PLAY & WIN. Zaidi ya HaloPoints, wateja pia wanaweza kufanya malipo ya tiketi za michezo hii kwa kutumia HaloPesa au Muda wa maongezi kupitia *150*88 #”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad