ANTONIO Conte ambaye aliwahi kuzipa ubingwa timu kubwa duniani ikiwa ni pamoja na Inter Milan na Juventus kwenye Serie A pamoja na Chelsea ndani ya Ligi Kuu England anatarajiwa kusaini dili jipya leo Jumanne ili kuweza kuwa Kocha Mkuu wa Tottenham.
Conte anakwenda kuchukua mikoba ya Nuno Espirito ambaye alichimbishwa mazima jana Novemba Mosi akiwa ameongoza timu hiyo kwenye mechi 17 akishinda 9, sare moja na kupoteza mechi 7.
Espirito alifungashiwa virago kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ambapo kwenye mechi zake sita za Ligi Kuu England alipoteza mechi nne na aliibuka hapo Juni 30,2021 akichukua mikoba ya Jose Mourinho aliyefutwa kazi Aprili 19,2021.
Kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester United akiwa nyumbani kiliwafanya mabosi wa timu hiyo kushindwa kuvumilia na kufanya iwe ni rekodi ya kumtimua kocha wa nne ndani ya miaka mitatu na Conte anatajwa kupewa dili la miezi 18.

No comments:
Post a Comment