PRESHA imezidi kuwa kubwa ndani ya Simba kutokana na matokeo ambayo wanayapata na kuelekea katika mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC kuna nyota kadhaa ambao wataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa Chris Mugalu, Pape Sakho, Mzamiru Yassin, Taddeo Lwanga ni miongoni mwa nyota watakaokosa mchezo dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Mchezo uliopita ilikuwa dhidi ya Coastal Union na waligawana pointi mojamoja kwa sare ya bila kufungana

No comments:
Post a Comment