SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa walitengeneza nafasi nyingi ila haikuwa bahati yao kwa ajili ya kufunga mabao ambayo yangewapa ushindi.
Kwa upande wa Coastal Union, Kocha Mkuu, Melis Medo amesema kuwa ishu ya wachezaji wake kuonyeshwa kadi za njano pamoja na nyekundu kwa mchezaji wake Benedict sio ishu ya nidhamu bali waamuzi wana majibu kuhusu hilo.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Simba 0-0 Coastal Union
No comments:
Post a Comment