PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa watatumia
uzoefu ambao wamepata kwenye mechi za kimataifa kuweza kuwakabili Yanga kwenye
mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.
Yanga ilitangulia katika hatua ya robo fainali kwa ushindi
mbele ya Geita Gold hivyo itakutana na Simba katika mchezo wa nusu fainali Mei
28,Uwanja wa CCM Kirumba.
Pablo amesema kuwa lengo
la kwanza ilikuwa ni kuweza kutinga hatua ya nusu fainali kisha ushindi
utafuata.
“Tumecheza mechi ngumu na zenye ushindani mkubwa katika
mashindano ya kimataifa, (Caf) hivyo uzoefo wa mechi hizo kubwa utatufanya
tuweze kupata matokeo kwenye mchezo ujao.
“Kitu kizuri ni kwamba tumeshinda na tunakwenda mbele katika
mashindano haya, tutakutana na Yanga katika mchezo wetu wa nusu fainali hilo
lipo wazi hivyo ninajua kwamba tutapata muda wa kufanya maandalizi,”.
Zimebaki siku mbili kabla ya watani hawa jadi kuweza
kukutana katika msako wa ushindi wa timu itakayokwenda hatua ya fainali.
No comments:
Post a Comment