YANGA YAANZA KWA KUPOTEZA KIMATAIFA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 25 November 2023

YANGA YAANZA KWA KUPOTEZA KIMATAIFA

 


KATIKA mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kutoka Tanzania wawakilishi wameanza kwa kupoteza pointi tatu ugenini.

Ni kwenye mchezo uliochezwa usiku kuamkia leo Novemba 25 Yanga ilitupa kete yake ya kwanza ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ilikuwa imara kwenye umiliki wa mpira na pasi nyingi ila wapinzani wao walicheza kwa mbinu ya kusaka ushindi.

Mwisho baada ya dakika 90 ubao ulisoma CR Belouizdad 3-0 Yanga na langoni alianza kipa namba mbili Metacha Mnata huku ukuta ukiwa na Dickson Job, Bacca waliokuwa na kazi ya kuzuia hatari za wapinzani wao.

Ni Benguit dakika ya 10, Bantahar dakika ya 45 na lile la tatu lilijazwa kimiani na Jallow dakika ya 90.

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa taji hilo la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 2 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad