SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 25 November 2023

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA


 AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa watawafurahisha mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mchezo wao dhidi ya ASEC Mimosas pamoja na wale watakaokuwa nyumbani.

Ipo wazi kwamba Novemba 25 Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

 Ally amesema kuwa wana kibarua kizito kwenye mchezo wao wa kimataifa lakini mipango yao ni kuwapa furaha mashabiki kwa kutoa burudani na ushindi mzuri.

“Tumetoka kwenye mechi ambazo zilikuwa ngumu na matokeo hayakuwa rafiki kwetu. Sasa kuelekea mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas tutawafurahisha Wanasimba wote kwa kupata ushindi.

“Ni mchezo muhimu kwa kila mmoja, wachezaji wanalitambua na maandalizi yanaendelea hivyo ambacho kipo ni utayari na mashabiki kuzidi kushikamana katika hilo,” amesema Ally.

Kwenye mchezo wa leo kuna hatihati ya kukosekana kwa kiungo Clatous Chama kwa kuwa alichelewa kurejea kambini akitokea Zambia alipokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Aishi Manula kipa namba moja wa Simba bado hajawa fiti pia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad