ANUARI Mosi,2024 Neema ya Mungu imetuzunguka na kutufanya tuwe hapa kwa wak
ati mwingine katika hili tunapaswa kusema asante.
Hakika ni wakati mwingine mzuri kwa ajili ya kuanza kupambania malengo ambayo yalianza kuandikwa tangu wakati ule unapambania yale unayohitaji.
Kwenye ulimwengu wa mpira kila timu imefunga kwa mpango wake katika mechi za funga mwaka na wengine wana kazi kwenye mechi za kufungua mwaka hapo ina maana kwamba majukumu bado yanaendelea.
Tunaendelea kukumbushana kuhusu kila mchezaji kuwa mlinzi wa mchezaji mwingine ndani ya mwaka mpya wa 2024 na mapinduzi katika hili yanapaswa kuonekana kwa vitendo.
Wachezaji wamekuwa wakiendelea kufanya matukio ambayo yanakuacha mdomo wazi na muda mwingine unashindwa kuwa na chaguo.
Kwa nini mchezaji umchezee faulo mbaya wakati unaweza kumlinda na kumfanya azidi kutimiza majukumu yake ndani ya timu.
Kumbuka kwamba kwa 2023 wapo ambao walikwama kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi kutokana na kutibu matatizo ambayo walikuwa nayo hivyo 2024 kuwe na mabadiliko katika hili.
Furaha na amani zizidi kutawala kwenye ulimwengu wa mpira huku ushindani ukizidi kupasua anga hili ni jambo la muhimu kwa kila mmoja kuzingatia.
Hakuna timu ambayo inaingia uwanjani ikiwa haina hesabu za kushinda lakini hakuna mchezaji anayeingia uwanjani akiwa na hesabu za kumuumiza mchezaji mwingine pia.
Wakati huu wa mwanzo wa Januari ikiwa ni ukurasa wa pili ndani ya 2024 basi ni muda mzuri wa kutafakari na kufanya kweli kuhusu kucheza kwa utulivu na kufuata kanuni ambazo zipo kwenye mpira.
Hakuna ambaye anapenda kumuona mchezaji mwenzake akiwa ameumia hilo lipo wazi lakini inapotokea hakuna mpira basi haina haja ya kucheza faulo isiyo ya lazima.
Wakati mwingine mchezaji anamchezea mchezaji mwingine faulo ilihali mpira hana maana ya kuwa na mwendelezo kwa wakati huu 2024.
Ni wakati mwingine wa kuendelea kuwa walinzi wa wachezaji ndani ya uwanja ili kuwapa fursa ya kutimiza majukumu yao uwanjani.
Kwenye matumizi ya nguvu huwezi kuzuia kwa kuwa hata kupiga mpira wenyewe kupeleka upande mwingine kunahitaji nguvu hilo haliepukiki.
Kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup ni muhimu kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa wakati tunaona namna ambavyo hali ilivyo pamoja na ushindani uliopo.
Wakati uliopita wachezaji walikuwa wanaumia mashindano yanapofika ukingoni na kuwa ni hasara kwake na timu kiujumla.
Mapinduzi ya mwaka huu ikawe ni tofauti kwa kila timu kucheza kwa umakini kusaka ushindi kwani raha ya dakika 90 ni kupata mshindi na mwisho kila mmoja anaedelea na maisha yake ya kawaida.
Ile vita ya kisasi kwa 2023 iwekwe kando bali uwe ni muda wa kufanya mapinduzi ya kweli kwenye ulimwengu wa mpira.
Wachezaji kikubwa ambacho kinatakiwa ni kushinda mechi kwa kupata matokeo mazuri na ili hayo yatokee ni lazima kila mmoja afanye maandalizi mazuri.
Muda uliopo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi sio mrefu sana tofauti na ligi ambayo inaendelea kwa muda mrefu kukamilisha ngwe zote ikiwa ni ya mzunguko wa kwanza na ule wa pili.
Basi ikawe ni mashindano yatakayoongeza mvuto na kila mchezaji kutimiza majukumu yake kwa umakini.
Ikumbukwe kwamba dunia inafuatilia mashindano haya kupitia Azam TV hivyo hakuna tatizo kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao wote lakini wakumbuke kulindana ndani ya dakika 90.
Wale ambao wanaamini kwamba hawawezi jambo hilo wana muda mzuri wa kuzungumza na benchi la ufundi ili wapewe umuhimu wa kucheza kwa umakini.
Iwe ni 2024 yenye mafanikio, kheri na furaha kwenye kila hatua kwa wale ambao wameanza kwa mtindo wa kipekee tofauti na wengine basi tunawaombea kher ili waendelee na gurudumu la kusaka maendeleo.
ReplyForward Add reaction |
No comments:
Post a Comment