FAINI ZATEMBEA SIMBA NA YANGA, ISHU YA USHIRIKINA YAWAPONZA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday 15 February 2024

FAINI ZATEMBEA SIMBA NA YANGA, ISHU YA USHIRIKINA YAWAPONZA

 


KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu nchini imezitoza faini ya jumla ya shilingi milioni tano Simba na Yanga kutokana na makosa mbalimbali yaliyojitokeza kwenye baadhi ya michezo iliyopita ya NBC Premier League.


Katika faini hiyo Simba imetozwa jumla ya shilingi milioni tatu ambapo milioni moja ya kwanza ni kosa la mashabiki wake kuonekana wakimwaga vitu vyenye asili ya unga katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wakati wa mchezo dhidi ya Tabora United, kosa la pili ni mashabiki wa timu hiyo kurusha chupa wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC.

Na milioni moja ya mwisho ni kutokana na mashabiki wa timu hiyo kuingia kwenye eneo la kuchezea baada ya mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga SC wao wametozwa jumla ya shilingi milioni mbili kutokana na tukio la mashabiki wa watatu (3) wa timu hiyo kuonekana katika eneo la vyumba vya kuvalia kuelekea mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya na kosa la mwisho ni kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuchelewa kurudi uwanjani kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika taarifa hiyo pia mchezaji wa Tanzania Prisons, Zabona Mayombya amefutiwa kadi ya pili ya njano iliyozaa kadi nyekudu aliyopata katika mchezo wao dhidi ya Yanga.

Pia Wachezaji wawili wa Klabu ya Yanga, Kibwana Shomari na Clement Mzize, wamepigwa faini ya shilingi milioni 1 kila mmoja, baada ya kukutwa na hatia katika makosa ya kufanya vitendo vinavyoashiria ushirikina.

Taarifa imeeleza kuwa Clement Mzize ali alionekana akitoa taulo la mlinda mlango wa Klabu ya Dodoma Jiji lililokuwa limewekwa kwenye lango la timu hiyo katika mchezo kati ya Yanga na Dodoma Jiji.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Kibwana naye alionekana akiondoa taulo la mlinda mlango wa Mashujaa katika mechi kati ya Yanga na Mashujaa, jambo linaloashiria imani za kishirikina..

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad