SIMBA YATAMBA KUENDELEZA DOZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday 16 February 2024

SIMBA YATAMBA KUENDELEZA DOZI

 


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa utaendelea kutembeza dozi kwenye mechi ambazo watacheza kitaifa na kimataifa.

Chini ya Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha kikosi cha Simba kilikamilisha mzunguko wa kwanza kwa kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-1 Simba.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na kiungos mshambuliaji Clatous Chama dakika ya 33 likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Matheo Anthony na Sixtus Sabilo wa JKT Tanzania walikuwa kwenye ubora wao na walikuwa na nafasi za kufunga lakini mikono ya Ayoub Lakred na ulinzi wa Che Malone ulilifanya lango la Simba kuwa salama.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wanawapongeza wachezaji kwa kujituma kwenye mechi zao na wanaamini wataendelea kufanya hivyo kwenye mechi zijazo.

"Pongezi kwa wachezaji kwa kuwa wanapata ushindi kwenye mechi ngumu zenye ushindani na hili linapaswa kuwa endelevu kwa kuendelea kutoa dozi kwenye mechi zetu zijazo, tunaamini itakuwa hivyo,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad