WAPAMBANAJI katika Kombe la Shirikisho, Simba leo
Februari 13 wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya
Ivory Coast.
Ushindi huo unawafanya waongoze kundi wakuiwa na pointi tatu na mabao matatu kibindoni na wamefungwa bao moja.
Bao la mapema lilijazwa kimiani na Pape Sakho ilikuwa dakika ya 12 kwa pasi ya Shomari Kapombe lilidumu mpaka muda wa mapumziko.
Kipindi cha pili ASEC Mimosas walifanya kweli na kupata bao la
kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Aziz Stephan ambaye alitumia vema
makosa ya safu ya ulinzi wa Simba chini ya Joash Onyango.
Bao la pili kwa Simba lilipachikwa na Kapombe ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti moja matata ilikuwa dakika ya 78.
Iliwachukua dakika tatu mbele Simba kupachika bao la tatu kupitia
kwa Peter Banda ambaye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kuvua jezi
wakati anashangilia.
Licha ya ushindi huo ASEC Mimosas walionekana wazuri katika umiliki
na waliweza kufanya hivyo kwa asilimia 52 huku Simba ikiwa ni asilimia
48.
Mchezo wao wa marudio unatarajiwa kuchezwa Machi 20 nchini Ivory Coast hivyo Simba bado wana safari ndefu katika kundi D katika Kombe la Shirikisho.
No comments:
Post a Comment