MECHI za awali zimeanza kwenye mechi za kimataifa na tunaona wawakilishi wa Tanzania wameanza kupata matokeo chanya katika mechi za awali.
Pia zipo ambazo zimepata matokeo ambayo walikuwa hawayahitaji
wala kuyatarajia ni muhimu kupanga mipango upya kwa ajili ya mechi zijazo.
Kila hatua ambayo inapigwa ni muhimu kufanya maandalizi mazuri
kwa kuwa hakuna matokeo yanayopatikana kwa kufikiria bila utendaji wa kazi
uwanjani.
Hapa tunaona kwamba wawakilishi kwenye mechi za kimataifa kila
mmoja anapeperusha bendera ya Tanzania akiwa na malengo ya kupata matokeo
mazuri.
Inawezekana lakini kama hakutakuwana mipango makini baada ya
kumaliza mchezo mmoja kutakuwa na matokeo mengine tofauti na vile ambavyo
mashabiki na uongozi wa timu husika unahitaji.
Kwa namna ambavyo timu itakuwa imeweza kufanya maandalizi yake
itakuwa kwenye namna yake ya kupata matokeo.
Kwa kilichopatikana kwenye mechi za wakati huu ni mpango kazi
uliopangwa wakati uliopita kwa kazi iliyokuwa inafanywa kwenye uwanja wa
mazoezi.
Msimu mpya kimatifa ni wakati mpya wa kufanya mambo mengine
tofauti na wakati uliopita hiyo itawafanya kila mmoja apate matokeo chanya.
Ipo wazi kwamba maisha yakwenye mechi za kimataifa yana utofauti
mkubwa na maisha ya ligi hasa kwenye upande wa mashindano husika na aina ya
mechi ambazo zinachezwa kuwa na ushindani mkubwa.
Wachezaji kazi yao ni moja kufuata maelekezo ya benchi la ufundi
ili waweze kupata kile wanachokistahili,kikubwa ni mipango kazi na ushirikiano.
Ni wakati mzuri wa kujipanga tena na timu kuangalia yale ambayo
waliweza kuyafanya msimu uliopita na kushindwa kufikia malengo ambayo walikuwa
wamejiwekea kitaifa na kimataifa.
Kupata matokeo kwenye mechi za awali ni hatua kubwa na itazidi
kuongeza hali ya kujiamini kwa timu husika kwenye kutafuta matokeo uwanjani.
Tanzania inakwenda kupeperushwa na timu nne ambazo nina amini
zote zina uwezo mkubwa na visiwani Zanzibar pia kuna timu mbili ambazo
zinapeperusha bendera muhimu timu zote zikawa na matokeo chanya.
Fursa nyingine kwa wachezaji kuwa sokoni kwenye anga la
kimataifa hili ni jambo kubwa ambalo litawafanya wazidi kuimarika na kuwa na
thamani zaidi sokoni kitaifa na kimataifa.
Ipo wazi kwamba mashindano ya kimataifa yanahitaji maandalizi
mazuri ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye kila mechi.
Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba kwenye mashindano ya
kimataifa kwa mara nyingine tena kuona kila mmoja anashindwa kusonga mbele.
Wapinzani nao wanatambua kinachohitajika ni matokeoya ushindi
iwe mechi inachezwa ugenini ama nyumbani inawezekana kushinda.
Nina amini kwamba wachezaji ambao walishawahi kushiriki
mashindano ya kimataifa wanaona namna wanavyozidi kupata uzoefu kwenye
kila hatua na hili ni jambo zuri.
Kadri ambavyo wanaata nafasi ya kucheza kimataifa wanangeza hali
ya uzoefu kwa wale wazawa inakuwa kazi nyingine ya kuongeza hali ya kujiamini
pale watakapoitwa timu ya taifa ya Tanzania kutimiza majukumu mengine.
Jambo la muhimu ni maandalizi mazuri kwa mechi na kupata
matokeo, wachezaji jitoeni bila kuogopa kwa ajili ya kupambania timu na
kutimiza majukumu yenu.

No comments:
Post a Comment