LIVERPOOL YAAMBULIA POINTI MOJA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 4 September 2022

LIVERPOOL YAAMBULIA POINTI MOJA

 


LICHA ya kuwa na mastaa wake wote ndani ya kikosi cha Liverpool ikiwa ni Mohamed Salah, Roberto Firmino, Virgil Van Djik waliambulia pointi moja mbele ya Everton kwenye Merseyside Dabi.

Unakuwa ni mchezo wa tatu kwa Liverpool kupata sare msimu huu ikiwa imecheza mechi sita, imeshinda mbili na ilinyooshwa mbele ya Manchester United.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Goodison, Everton bao lao ambalo walifunga kwenye mchezo huo lilifutwa baada ya teknolojia ya VAR kueleza kuwa ilikuwa ni bao la kuotea.

Jumla yalipigwa mashuti 37 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Matokeo hayo yanafanya Liverpool kufikisha pointi 9 nafasi ya 6 huku Everton wakifikisha pointi nne nafasi ya 16.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad