MOSES Phiri mshambuliaji wa Simba ameweka wazi kuwa wanahitaji kuendelea kufunga kwenye mechi ambazo wanacheza jambo ambalo linawapa furaha.
Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kwenye mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets, ubao ulisoma Nyasa Big Bullets 0-2 Simba.
Phiri ni miongoni mwa nyota wa Simba ambaye alifunga moja ya mabao bora CAF dhidi ya Big Bullets amesema anapopata nafasi ya kufunga atafanya hivyo anahitaji kufunga mabao mengi.
"Ninacheza ndani ya Simba timu yenye uimara na ushindani mkubwa wa namba kwenye kila hatua hivyo ambacho ninakifanya kila nikipata nafasi ninapambana kufunga.
"Tunahitaji kuona tunapata matokeo kwenye mechi zetu na kila kitu kinawezekana ikiwa tutashirikiana na kufanya kazi kwa nguvu bila kukata tamaa," amesema.
Kikosi cha Simba kimerejea Dar kikitokea Malawi na Phiri ni miongoni mwa mastaa ambao walikuwa kwenye msafara huo.

No comments:
Post a Comment