MTAALAMU WA PENALTI KARUDI YANGA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 6 September 2022

MTAALAMU WA PENALTI KARUDI YANGA


MTAALAMU wa mapigo huru ndani ya kikosi cha Yanga Tuisila Kisinda amerejea na kuongeza orodha ya watakaokuwa na kazi ya kufanya hivyo ndani ya kikosi hicho.

Kisinda msimu wa 2020/21 ndani ya Yanga alikuwa na majukumu ya kupiga penalti na kwenye mabao manne aliyofunga msimu huo ni mawili alifunga kwa penalti huku mawili akifunga kwenye mwendo wa kawaida.

Nyota huyo alihusika kwenye mabao 7 kati ya 52 yaliyofungwa na timu hiyo iliyogotea nafasi ya pili na pointi 74.

Aliwafunga kwa mkwaju wa penalti KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba dakika ya 40 pia aliwatungua Kagera Sugar bao moja kwa mkwaju wa penalti ilikuwa Uwanja wa Mkapa dakika ya 13.

Licha ya uwezo huo aliwahi kukwama kuwatungua Coastal Union kwa penalti kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Machi 4,2021 wakati Yanga ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 ambalo bai la Yanga lilifungwa na Kisinda mwenyewe.

 Bao lingine staa huyo mwenye spidi 120 akiwa uwanjani aliwatungua Mwadui FC, Uwanja wa Kambarage dakika ya 56.

Mbali na uwezo wa kupiga mapigo huru pia ana uwezo wa kutengeneza nafasi ambapo aliweza kutoa pasi tatu za mabao alitoa pasi ya bao kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, alitoa pasi mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Ataungana na Aziz KI, Bernard Morrison na Fiston Mayele ambao wamekuwa wakipewa majukumu ya mapigo huru ambapo Yanga ikiwa imecheza mechi mbili za ligi imepata penalti moja na mpigaji alikuwa Mayele aliyekosa mbele ya Polisi Tanzania dakika ya 11.

Kwa sasa nyota huyo usajili wake umezua utata baada ya jina lake kutoingizwa katika usajili kwa kuwa Yanga imetimiza usajili wa wachezaji wakigeni 12.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad