MWAKINYO KUZICHAPA LEO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 3 September 2022

MWAKINYO KUZICHAPA LEO

 


BONDIA kutoka Tanzania Hassan Mwakinyo leo Septemba 3,2022 anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na kwenye pambano la raundi 12.

 Jana Septemba 2, Mwakinyono aliweza kupima uzito huko jijini Liverpool nchini Uingereza akiwa tayari kushuka Ulingoni kuzichapa na Muingereza Liam Smith.


Pambano hilo linatarajiwa kuchezwa saa 3:00 usiku Jijini Liverpool, kwenye Ukumbi wa M&S Bank Arena ndani ya jiji hilo.

Katika zoezi hilo la upimaji uzito Mwakinyo  alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote mbele ya mpinzani wake Smith walipokuwa wakitazamana uso kwa uso.

Pambano hilo ni la uzani wa Super Walter, ambapo Mwakinyo alibainisha kuwa yupo tayari kwa ajili ya pambano la leo. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad