SIMBA:MAFANIKIO YA SIMBA HUWEZI KUMUWEKA KANDO GEMBE - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 4 September 2022

SIMBA:MAFANIKIO YA SIMBA HUWEZI KUMUWEKA KANDO GEMBE


PATRICK Rweyemamu, Meneja wa Simba ameweka wazi kuwa mafanikio ya timu hiyo huwezi kuyataja na kumuweka pembeni Dk Yassin Gembe.

Gembe alitangulia mbele za haki Septemba 2,2022 ambapo taarifa ilitolewa na uongozi wa Simba ilieleza Gembe aliyekuwa daktari wa timu ya wanaume (Senior Team) kilitokea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Leo Septemba 4, imefanyika ibada ya kumuaga Gembe ambapo wachezaji na familia ya michezo imeweza kufika Mbweni kwa ajili ya kuhani msiba.

Rweyemamu amesema: "Sisi tuliobahatika kuishi na kufanya kazi na Dkt. Gembe tumepoteza mtu wa kipekee.

" Mafanikio ya Simba yaliyopatikana sasa hauwezi kumweka pembeni sababu alikuwa na mchango wake kuandaa timu kwenda kwenye mchezo," .

Miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao walikuwa kwenye kuaga mwili wa Gembe ni pamoja na Erasto Nyoni,Ally Salim,Sadio Kanoute.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad